DARAJA LA MWANZA LAWA MKOMBOZI
Na Zuleha Issa
SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, imepania kuifanya Mwanza kuwa kitovu cha usafi ri nchini kwani itaunganisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kuimarisha usafi ri wa ndege, reli na meli katika Ziwa Victori
Akizungumza katika uzinduzi wa daraja la kisasa la watembea kwa miguu la Furahisha na baadaye katika mkutano wa hadhara wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona, Nyakato, Rais Magufuli alisema hayo yanafanyika kama sehemu ya mchakato wa kuijenga Tanzania mpya kuelekea uchumi wa viwanda Mwanza ikiwa kitovu cha usafiri EAC.
Alisema katika kuhakikisha ukuaji wa jiji katika sekta ya viwanda, Serikali imekuwa ikipigania pia ukuaji wa miundombinu yake, ikiwemo ujenzi wa daraja la Furahisha, upanuzi wa uwanja wa ndege na jengo la kupumzikia abiria, lakini pia barabara za kutoka kwenda na kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza aliyoipanua kwa Sh bilioni mbili alizobana kutoka fedha za sherehe za Muungano alipoingia madarakani tu.
Daraja lilolojengwa mkoani Mwanza |
.
Alisema mchakato wa kumpata mzabuni kutoka Korea Kusini uko katika hatua nzuri. Utakaposainiwa hivi karibuni, inatarajiwa ujenzi wa meli hiyo mpya utafanyika na itachukua miezi 12 hadi kukamilika. Alisema ujenzi wa meli hiyo unatarajiwa kugharimu Sh bilioni 60 zitakazotolewa na Serikali kutokana na mapato yake ya ndani.
.
Hatua hizo ni utekelezaji wa ahadi ya rais huyo aliyoitoa kwa wananchi wa Mwanza wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015. Rais alisema ujenzi huo wa meli mpya unakwenda sambamba na ukarabati wa meli za MV Victoria na MV Butiama zilizopo hivi sasa.
MV Victoria inatarajiwa kukarabatiwa kwa miezi saba, kwa Sh bilioni 22 kutoka serikalini. Imeelezwa ukarabati huo utahusisha uwekaji wa injini mpya, jenereta, viti na upakaji rangi.
Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tani 200 kwa wakati mmoja, ilisimama kufanya safari kati ya Mwanza na Bukoba mwaka 2014 baada ya kuchakaa. Nayo MV Butiama yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na mizigo tani 100 kwa wakati mmoja, itafanyiwa ukarabati kwa miezi sita kwa gharama ya Sh bilioni tatu kutoka serikalini.
Aidha, kwa usafiri wa barabara kutoka Mwanza kwenda Kampala, Rwanda kupitia Nairobi ni kilometa kwa 717, wakati kwa ndege ni umbali wa kilometa 317. Kutokana na juhudi za Serikali za kutaka kupaisha uchumi wa Tanzania, Rais Magufuli ametoa mwito kwa Watanzania kwa jumla kushirikiana na serikali anayoiongoza kuijenga Tanzania ya viwanda na kuifikisha kwenye uchumi wa kati.
Huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kutokana na jihudi zake za kuhamasisha uwekezaji wa viwanda mkoani hapa, Rais alisema hatamvumilia mkuu wa mkoa atakayeshindwa kuchochea viwanda.
Akizindua kiwanda cha Sayona kilichojengwa na kampuni ya Kitanzania ya Motisan kwa gharama ya takribani Sh bilioni 11.8 chenye uwezo wa kuzalisha chupa 1,200 kwa dakika moja katika mitambo yake minne ya kuzalisha vinywaji baridi pamoja na chupa 100 za maji, Rais Magufuli amepongeza uwekezaji huo na kuwataka wafanyabiashara kuwekeza zaidi, akiahidi wataungwa mkono na Serikali.
Kiwanda hicho kimezalisha ajira za watu 200 na kinaungana na kiwanda kingine cha vinywaji baridi cha Sayona kilichopo Mboga, Bagamoyo mkoani Pwani kusindika matunda ya wakulima na kuinua hali zao za maisha.
Akizungumza baada ya Rais Magufuli kufungua kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Motisan Group, Subhash Patel alisema kampuni yake imedhamiria kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kujikita katika uchumi wa viwanda na ameahidi kuwa mwaka ujao wa 2018 kampuni hiyo itajenga viwanda vingine vitano.
Kuhusu ahadi yake ya kupeleka Sh bilioni 50 kila kijiji nchini, Rais alisema alisema ameona ni vyema zaidi kutumia mamilioni hayo kwa kuanza na uboreshaji wa huduma za afya, elimu, maji na barabara kwa manufaa ya Watanzania.
Post a Comment