MBOGA MBOGA ,MKOMBOZI KWA WANAWAKE KATA YA KITUNDA .
Kimama wa Kitunda wakiuza mboga zao katika soko la kivule. |
Dar
es salaam
Wanawake wa kata ya kitunda wameamua kuifanyia kazi
kwa vitendo kaulimbiu ya muheshimiwa raisi John Pombe Magufuri, ya hapa kazi tu
, kwa kujikita katika kilimo na biashara ya mboga mboga ili
kujikwamua kiuchumi .
Wanawke hao jana wakionge na mwandishi wetu walisema,wameamua kuacha kujibweteka nakuwa
magolikipa haili iliyo kuwa ikiwafanya wanyanyasike katika ndoa zao kwanii ili
wabidi wategemee kilakitu kutoka kwa waumezao ambao muda mwingine pia huwa
wanakosa kipato cha kuweza kumudu
kuhudumi familia zao nakupelekea kuwa na
maisha duni katika familia izao.
Walisema tangu waanze kujikita katika biashara hiyo sasa wanaweza
kusaidiana na wa umezao katika kuhudumia familia zao.
Bi.Tereza Mhando akiuza mboga zake katika soko la kivule |
Mwanamke mmoja aliye fahamika kwa jina la Tereza Mhando mkazi wa kipunguni B kata ya kitunda halimashauli ya
manispaa ya ilala alisema hapo mwanzo hakuwa ana jishughulisha na shughuli
yoyote alikuwa ni mama wanyumbani ambapo
alimtegemea mumewe katika kila kitu hali iliyo fanya kushindwa kumudu baadhi ya
mahitaji yake na ya watoto wake, lakini tangu alipo jikita katika kilimo cha
mboga mboga amepiga hatua kubwa kwani sasa anaweza kumudu hata kubadili mlo, kwani hapo mwanzo walikuwa wakila
mlo usio badilika ambapo alisema walikuwa wakila ugali maharage kila itwapo leo
,hivyo alitoa wito kwa wanawake wenzake kuinuka nakuacha utegemezi kwa waume zao kwani wanawake wanaweza tena sana kikubwa ni ujasili wa kufanya jambo na kutosikiliza maneno ya watu wanasema nini.
wanawake tufanye kazi utegemezi si kitu katika maisha ya sasa alisema Bi.Tereza Mhando
Post a Comment