Header Ads

PACHA WALIOSHIKANA KATIKA KICHWA WATENGANISHWA INDIA

Na. Zuleha Issa
Pacha walioshikana kichwani Jaga na Kalia
Mapacha Jaga na Kali walio ungana vichwa wakiwa wamefanyiwa upasuaji


Madaktari wa upasuaiji katika mji mkuu wa India Delhi wamefanikiwa kuwatenganisha wavulana pacha waliokuwa wameshikana katika kichwa.

Wavulana hao wa miaka miwili Jaga na Kalia walifanyiwa upasuaji uliochukua takriban saa 16 na sasa wako katika chumba wagonjwa mahututi ICU, kulingana na madaktari
.
Pacha walioshikana katika kichwa watengenishwa India
Pacha wakiwa tayari wamesha fanyiwa upasuaji
Habari kutoka nchini humo zinasema kuw akundi la madaktari 30 walifanya upasuaji huo katika taasisi ya matibabu na sayansi ya All India.

Wavulana hao walizaliwa wakiwa na wanatumia mishipa ya damu ya pamoja mbali na tishu za ubongo, hali isio ya kawaida ambayo hutokea mara moja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa.

No comments

Powered by Blogger.