Header Ads

SIGARA NA MADHARA YAKE KWA WANAMICHEZO


Dar es salaam.
MATUMIZI ya sigara katika jamii ni suala ambalo limekuwa likizungumziwa kila uchwao hii ni
kutokana na madhara yake kuwa makubwa katika afya binadamu,leo tujikite katika wachezaji
wa mpira wa miguu wanaojihusha na matumizi ya tumbaku yanavyoathiri sanaa yao ya michezo.
Sigara ina kemikali zaidi ya 4000 ndani yake ambapo kwa asilimia kubwa huathiri karibu viungo
vyote vya mwili wa binadamu ikiwemo mapafu,macho,pua,vidole vya mikono na miguu,maradhi
ya moyo na mengine mengi ambayo mtaalamu ameyafafanua.
 Hii inaonekana hata kwa mchezaji maarufu duniani Mario Baloteli raia wa Ufaransa mwenye asili ya Senegal, ambaye kiwango chake kimeshuka kutokana na matumizi ya uvutaji wa sigara.
Mario Baloteli kushoto akiwa na moja ya marafiki zake akivuta sigara.


Akizungumza na mwandishi wetu mapema wiki hii Dk Abel Amani alisema Mchezaji wa mpira
wa miguu anapojihusisha na matumizi ya sigara kiwango chake kinashuka pindi anapokuwa
uwanjani hii ni kutokana na mapigo yake ya moyo kwenda mbio na kumfanya ashindwe
kumudu mwili hali inayosababisha mshutuko wa moyo hata kifo
Pia matumizi ya sigara huathiri mfumo mzima wa hewa na mapafu hali inayomweka mchezaji
huyu kuugua saratani ya mapafu na kuziba kwa mfumo wa hewa ambapo huu ukionekana ni
ugonjwa utakaomfanya mchezaji huyu wa mpira kuitendea haki saana yake alisema Aman
Sigara husababisha mifupa kuwa nyepesi na kupunguza nguvu kemikali zilizopo ndani ya sigara
hupunguza uwezo wa mwili kujenga mifupa iliyo na nguvu na mifupa hii huvunjika kwa urahisi
na huchukua muda kupona.
Wapo watu ambao hujihusisha na kilevi hichi cha sigara bila kufahamu kwamba madhara
yanayopatikana huku ni makubwa kuliko kile wanachokitafuta katika kilevi hichi ikiwa wengi
hujidangaja sigara hupoteza mawazo na kupanua mapafu jambo ambalo sio sahihi ni upotoshaji
mtupu.
Sigara huweza kusababisha tatizo la kupasuka kwa vibofu vya hewa hali inayohatarisha afya ya
mchezaji pindi anapokuwa uwanjani,hii ni kutokana na uvutaji wa pumzi na uchezaji ni vitu
viwili vinavyoendana kwa karibu.
Kwa wachezaji wa mpira wa miguu ni muhimu wakatambua kwamba suala la kutunza afya yako
sio suala linalohitaji kuelezwa na kuelekezwa kwani utuzaji wa afya huweza kukufanya uwe na
viwango vizuri ikiwemo kuepuka matumizi ya vitu visivyokuwa vya lazima ambavyo huweza
kuigarimu afya yako ikiwemo ni kuepuka matumizi ya sigara.
Utafiti unaonyesha kila sekunde nane,mtu mmoja hufariki kutokana na matumizi ya tumbaku
hivyo upo umuhimu wa wachezaji mpira kuepuka matumizi haya ya sigara pamoja na jamii
nzima kwani hata katika vifungashiovya bidhaa hizi huwa wanaweka onyo ambalo ni rahisi
kuonekana.heshimu afya yako kwa faida yko binafsi na jamii inayokuzunguka.

No comments

Powered by Blogger.