MTANZANIA ANAYEKIPIGA UINGEREZA AANZA KWA MKOSI KATIKA TIMU YAKE MPYA.
Abbas Pira |
Mtanzani anayecheza soka
la kulipwa barani Ulaya Abbas Pira ameanza
kwa mkosi katika Timu yake mpya ya Wrexham F.C inayoshiriki ligi daraja la tatu
nchini Uingereza, baada ya kupata majeraha katika kifundo cha mguu wakati
wakicheza mechi dhidi ya Sutton United, mchezo ambao ulimalizika kwa kutoka
sare ya kufungana bao moja kwa moja.
Pira ambaye anacheza
nafasi ya golikipa katika Timu hiyo ya Wrexham F.C nchini Uingereza ambayo imemsajili
akitokea katika Timu ya United Leyton orient
Mlinda mlango huyo ameyapata
majeraha hayo baada ya kugongana na mshambuliaji wa Sutton United, Ntumba Massanka
wakati akiwa katika harakati za kuokoa goli katika lango lake.
Kwa mujibu wa madaktari
wa Wrexham F.C wamesema kuwa Pira akatakaa nje kwa muda wa miezi mitatu
akiendelea na matibabu katika hospitali moja ya Northwick nchini Uingereza.
Abbas Pira ambaye amepitia
Vilabu mbalimbali nchini Uingereza akianzia na Chelsea Academy kabla ya kwenda kukipika katika klabu
ya Birmingham city na hatimaye kutimukia Mk dons Colchester united, na kutokuwa
na maisha marefu katika klabu hiyo. Mpaka sasa anakipiga katika timu yake mpya
ya Wrexham F.C Inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini Uingereza.
Post a Comment