AGIZO LA RAIS MAGUFULI LATIMIA MKOANI MOROGORO
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli |
Morogoro
Agizo la Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli limetimizwa mara baada ya Mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka
13 wa shule ya msingi makutano iliyopo
wilayani kilombelo mkoa wa morogoro jinatuna
muhifadhi kusimamishwa masomo yake na kufukuzwa shule kutokana na kugundulika kuwa ana ujauzito.
Suala ambalo rais alilitilia mkazo siku za nyuma akiwa katika ziara yake mkoani Mwanza alisema
“Nikimuona Headmaster (Mwalimu mkuu), amemrudisha mwanafunzi aliyepata mimba, kwenye shule za Serikali, mwalimu huyo ataondoka,”
Haya yamejili mkoani morogoro baada zoezi la upimaji lililo endeshwa shuleni hapo
la kutambua wanafunzi walio pata ujauzito wakiwa shuleni.
Mwanafunzi akiwa na Ujauzito |
Daktari aliye julikana kwa jina moja la Lili alisema
kati ya wanafunzi 100 walio fanyiwa
kipimo hicho ni mwanafunzi mmoja pekee
aliye gundulika kuwa ni mjamzito.
Mwanafunzi huyo alipo hojiwa alidai kuwa alikuwa na
mahusiano na kijana aitwaye abdala shabaan mwenye umri wa miaka 27 ambaye
alitokomea kusikojulikana baada ya kubainika kwa tukio hilo.
Wazazi wa mtoto huyo walielezea tukio hilo kwa ma
sikitiko makubwa na baba wa mtoto huyo aitwaye
Lenfred Mlimandola alisema baada ya kupokea taarifa hizo alitoa taarifa polisi lakini mpaka jana
polisi walikuwa wakiendelea na upelelezi huku mtuhumiwa wa tukio hilo akiwa
hajulikani alipo.
Mwalimu mkuu wa shule ya makutano aitwaye Anna Suke alisema hatua zilizo
chukuliwa kwa msichana huyo ni kufutwa shule na alisema taarifa za kusimamishwa
masomo kwa mwanafunzi huyo tayari zimesha mfikia afisa elimu wa wilaya ya
kilombelo.
Afisa elimu wa Wilaya ya kilombelo Bwana John
Julius alidhibitisha kupokea taarifa
hizo naaliwaonya mabinti na kuwataka kuwa makini ili waweze kukamilisha ndoto zao wa wapo mashuleni, na kuachna na tabia za kujiingiza katika makundi hatarishi ambayo hayana maana yoyote katika taaluma yao.
Post a Comment