RAISI WA AWAMU YA PILI ALLY HASSAN MWINYI ANG’AKA MAUAJI YA WAZEE TANZANIA
Rais wa awamu ya Pili Ally Hassan Mwinyi akizungumza na wazee katika siku ya wazee Duniani iliyofanyika mkoani Dodoma |
Dodoma
Katika
maadhimisho ya siku ya wazee
duniani octoba mosi 2017 ,Raisi wa awamu
ya pili mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi
ameshangazwa na matukio ya
ukatili na mauaji dhidi ya wazee
kuendelea kukithiri nchini katika mwaka 2017. Aliyasema jana
wakati akihutubia katika siku ya wazee duniani ambayo maadhimisho yake
alifanyika Mjini Dodoma.
Rais Mwinyi alisema “niaibu na fedheha kubwa kuwa
mpaka sasa nchi yetu imeendelea
kushuhudia mauaji dhidi ya wazee”.
Aidha Rais Mwinyi aliwaahidi wazee mkoani dodoma kuwa
angefikisha ujumbe kwa serikali kutungia
sheria sera ya wazee ya mwaka 2013 ili
wazee waweze kupata haki na stahiki zao.
Katika maadhimisho hayo mkoani humo mwenyekiti wa chama cha wazee mkoani Dodoma
bwana Sebastiani aliiyomba
serikali kuendelea kutoa kipaumbele katika kutatua changa moto zinazo wakabili
wazee nchini.
Pia waziri wa maendeleo jinsia wazee na watoto Ummy
Mwalimu amemuahidi Mheshimiwa Mwinyi kuwa serikali itatekereza kikamilifu sera ya wazee ya mwaka
2013 pia itaendelea kutoa kipaumbele katika kutatua changamoto zinazo wakabili
wazee nchini.
Post a Comment