Header Ads

ZIARA CLOUDS YA ZUA SINTO FAHAMU MIONGONI MWA WANAFUNZI


Dar es salaama,
Ziara ya kutembele vyombo vya habari, ambayo imeandaliwa na chuo cha Uwandishi wa habari cha TIME SCHOOL OF JOURNALISM ( TSJ ) imezua sinto fahamu kwa baadhi ya wanafunzi waliokwenda katika kituo cha CLOUDS  habari.
Sinto fahamu hiyo ilizuka mara baada ya wanafunzi kufika katika maeneo ya kituo hicho yaliyopo mwenge cocacola na kukaa nje kwa muda wa saa moja na nusu bila ya kuingia ndani na kutomwona  mwalimu wao ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu, huku  ikidaiwa kuwa kuna program  inaendelea.
John shemaghoda ni  Miongoni  mwa wanafunzi walikuwa katika tukio hilo, ambapo waliachwa bila mwongozo wowote ule alisema ‘‘ Msimamizi wetu nani sasa?  hayo ndo maswali ambayo najiuliza, maana tumekaa hapa nje kwa muda mrefu kweli, isitoshe mvua inanyesha lakini hatumwoni yoyote mpaka sasa kutupa mwongozo unaendaje huko ndani, mategemeo yangu mpaka sasa nimuone mwalimu anatupa mwongozo, lakini ajabu mwalimu mwenyewe mpaka sasa haonekani na hatujui alipo.’’
Akizungumza na waandishi wa habari jana Rais wa chuo hicho Sabore Lazier alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo tulijaribu kuwasiliana na wahusika ilikujua taratibu zinaendaje, baada ya muda walikubali waingie watu thelathini tu kwa makubaliano yao na uongozi wa chuo, ikiwa sisi tulikuwa tupo sabini na nne.
‘‘kwanza nikiri kutokea kwa tukio hilo lakini nimejaribu kuliweka sawa na wote tuliingia na tulijifunza vitu mbalimbali jinsi ya kuandaa taarifa ya habari, kuandaa vipindi na uhariri wa habari pamoja na picha.
‘‘tulikuwa na mwalimu ambaye yeye ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu katika mambo yote lakini aliondoka mapema sana kabla hatujafanikiwa  kuingia katika lango la Clouds, aliniaga alisema anamatatizo kidogo yametokea yapo nje ya uwezo wake, hivyo mimi nilisimamia taratibu zote mpaka mwisho na kuliweka sawa jambo hilo,’’alisema Sabore
Alimalizia na kuwaomba wanafunzi wote kuwa mstari wa mbele, pindi ziara kama hizi zinapotokea. Kwani kuna mengi ya kujifunza ikiwa bado sisi ni wanahabari wachanga na kujua changamoto zilizopo katika  Tasinia ya Habari, hivyo tutumie muda wetu vizuri ilitwende na wakati katika kujua weredi wa mwanahabari aweje.

No comments

Powered by Blogger.