MVUA YASABABISHA MAAFA MUMBAI NCHINI INDIA
Daraja liliporomoka Mumbai nchini India kufuatia mvua kubwa ilikuwa ikinyesha. |
Watu kumi na wawili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, kufuatia kuwapo kwa mkanyagano baada ya daraja moja kuporomoka karibu na kituo cha treni, mjini Mumbai India.
Msemaji wa shilika la reli Anix
Saxena amezungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa daraja hilo lililofunikwa
lillikuwa na shughuli nyingi kutokana na idadi kubwa ya wasafiri walio kuwa
wanajikinga na mvua kwa pamoja katika
daraja hilo na hivyo kupelekea daraja kuzidiwa
uzito na mwishowe kuporomoka.
Waliyoshuhudia wanasema, daraja hilo
huenda liliporomoka kutokana mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati huo, hali
ambayo iliwafanya watu kukimbilia mahali hapo kwaajili ya kujikinga na mvua.
Hatahivyo habari kutoka nhini humo
zinasema kuwa mamlaka imekuwa ikilaumiwa
kwa kutelekeza miundo mbinu katika mji huo licha ya kuwa mji huo unapokea watu
wengi kila siku.
Aidha Watu waliojeruhiwa
wamefikishwa katika hospitali iliyo karibu na maafisa wakuu wa reli na uchuguzi
zaidi wa tukio hilo unaendelea
Post a Comment