Header Ads

WANAWAKE SAUDI ARABIA WARUHUSIWA KUENDESHA MAGALI.



Mwanamke mmoja nchini Saudi Arabia akiendesha gari baada ya mfalme wa nchi hiyo kutoa ruhusa kwa wanawake kuendesha magari nchini humo.

Riyad, Saudi Arabia.
Hatimaye wanawake nchini Saudi Arabia wameruhusiwa kuendesha magari jambo ambalo lilipigwa marufuku kwa mda mrefu nchini humo huku wanawake hao wakidai haki hiyo kwamda mrefu bila mafanikio.

Kwa mujibu wa habari kutoka nchini humo zinasema kuwa mfalme wanchi hiyo Bwana Salman bin abbdulaziz al saud ametoa ruhusa hiyo kwa wanawake kuendesha gari jambo ambalo halikuwapo hapo awali kwani ilikuwa  akionekana mwanamke anaendesha gari anatozwa faini kwa kosa hilo.
Saudi Arabia ni nchi pekeeambayo ilikuwa hairuhusu mwanamke kuendesha gari na hivyo kupelekea nchi nyingine kuitafsiri nchi hiyo kuwa inamnyonya mwanamke katika kumpatia haki zote anazo stahiki mwanadamu .

 
Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin abdulaziz al saud.
Kwani awali wanawake hawakuruhusiwa kupiga kula na kuendesha gari hivyo kufuatia tamko hilo la mfalume salman limefanya watu wa mtafsiri kama ni moja ya mtu anaependa maendeleo ya wanawake na hivyo kujizolea sifa nyingi juu ya uamuzi aliouchukua.

Aidha Dornard Trump ameipongeza  Saudi Arabia kwa uamuzi huo kwa kile alichodai kuwa utasaidia katika kuwa inua wanawake nchini humo na ukizingati technologia imezidi kuimalika hivyo kufanyahivyo kutasaidi kukuza uchumi wanchi yao sambamba na kuwapati haki  hiyo muhimu wanawake hao.   

No comments

Powered by Blogger.