PAMBA YAWA KIZUNGUMKUTI SOKONI.
Pamba ikiwa shambani bado kuvunwa mkoani Shinyanga. |
Simiyu.
Kufuatia kwa kuwepo kwa tabia ya baadhi ya wakulima
wa pamba kuongeza uzito wa pamba kwa kuziwekea maji, mawe na hata mchanga ili
pamba hizo ziwe nzito wakati wanapozifanyia kipimo imepelekea kupanda kwa bei
ya pamba.
Akizungumza kwenye uzinduzi wazao hilo uliofanyika kijiji
cha mwabusalu wilayani Meatu mkuu wa
mkoa wa shinyanga Zainabu Terack amesema bei ya pamba kilomoja imepanda kutoka
1000 mwakajana kufikia 1200 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Terack akizungumza na Wananchi. |
Terack aliwaataka wakulima hao kuacha kufanya hivyo kwani kufanya hivyo kuna punguza thamani ya zao hilo na hivyo kupelekea kushaka kwenye soko la dunia.
‘’Serikali imejipanga kuhakikisha inawakamata na
kuwachukulia hatua wale wotewatakao bainika kuchafua zao hilo,ni vyema kuvuna
na kuuza pamba safi’’alisema Terack.
Pia aliwataka wanunuzi kuhakikisha mizan iimehakikiwa
na wataalam wa vipimo iliwasiwaibie wakulima na kwamba watakao bainika
watachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kuhukumiwa papo kwa papo na mahakama
inayo hishimika.
Nae mkurugenzi wa bodi ya pamba Tanzania [TCB] Marko
Mtunga alisema wanatarajia kununua tani milioni1 zapamba nchi nzima.
‘’Matarajio hayo yamekuja kufuatia kushuka kwa
uzalishaji kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,na kwakuwa wakulima walikata
tamaa ya kuendelea kuzalisha pamba ndomana tumeamua kufanya hivyo.’’alisema
Marko.
Post a Comment