Header Ads

MWANAMKE MWEYE ULEMAVU AFANYIWA KITENDO CHA UKATILI

DAR ES SALAAM
Kutothaminika kwa mwanamke katika jamii na kuonekana hana mchango wowote na kufanyiwa ukatili wa kijinsia kwa wale wenye ulemavu na  unyanyasaji ni changamoto ambayo tunaishi nayo katika mazingira yetu nchini Tanzania.
Hayo aliyasema Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Msimbazi bonde Ndugu Ernest Msichoke ofisini kwake, baada ya kuhojiwa na mwandishi wetu juu ya sakata la kubakwa kwa mwanamke huyo mwenye ulemavu wa viungo (jina tuanalihifadhi) lililotokea siku tatu zilizopita katika eneo hilo.
“Ni kweli tukuo hili limetokea katika eneo langu lakini kitendo hiki si cha kuvumilika hivyo kama serikali ya mtaa na kwa kushirikiana na jeshi l polisi tumekwisha anza msako kwa watu wote waliohusika na kitendo hiki cha ukatili, kwa maana mama Yule mlemavu wa mikono hana hatia yoyote, wananchi pia watoe ushirikiano mzuri kwa jeshi la polisi katika kutoa taarifa sahihi juu ya watu hao”alisema  Ndugu Ernest Msichoke
Hata hivyo kwa upande wa wananchi nao walisikitishwa na kitendo hicho cha ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mwanamke mlemavu na kuiomba serikali pamoja na vyombo vya sheria kulitilia mkazo suala hilo na kuwatia nguvuni wote wanaohusika na suala hilo.
Bi.Asha Charles ni moja kati ya wanawake ambao ni wanaharakati wa haki za kibinaadam ambaye anafanyakazi katika ofisi ya serikali ya mtaa huo wa msimbazi bondeni kitengo cha dawati la jinsia Alisema“ sheria za haki za kibinaadamu zinapinga vikali ukatili wa kijinsia kwa wanawake, tena siku izi ukatili wa kijinsia kwa wanawake wenye ulemavu ndiyo umechukua nafasi kubwa sana katika jamii, niwaombe jamii kwa ujumla kutovumilia vitendo hivi katika maeno yao kama wakisikia jambo baya linamkumba mwanamke"
Aidha Bi.Asha Charles aliwataka wanawake wote wa eneo hilo kufika katika ofisi na kitengo chake cha dawati la jinsia ilikupata ufafanusi mzuri juu ya sheria za haki za kibinaadamu na haki za mwanamke juu ya suala zima la ukatili.
Hata hivyo mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo waliwaomba juu ya kuimalishwa kwa ulinzi shirikishi katika maeneo yote ambayo ni hatarishi hasa nyakati za usiku pindi watu wanaporudi makazini. Mwisho kabisa alimwomba mwanaharakati Bi.Asha Charles kutoa elimu ya jinsia kwa wakazi wote wa eneo lake ilikuweza kupata uwelewa mkubwa juu ya Elimu ya kijinsia na kuondokana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake wenye ulemavu wa viungo.

No comments

Powered by Blogger.