WAZIRI UMMY; MAZOEZI NI MUHIMU
Waziri wa Afya, jinsia wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam |
Imeelezwa kuwa watu wengi wamekuwa wavivu kufanya mazoezi hasa kwa wale wanaoishi mijini na wanaofanya kazi za kukaa muda mrefu maofisini na kujikuta wakitumia usafiri wa magari binafsi na kujiweka katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali.
Ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara kwa mtu ni mambo muhimu sana katika maisha ya binadamu
yeyote bila kujali umri,jinsia au kabila suala la mazoezi ni jukumu la kila mtu.kwa manufaa ya afya yake binafsi na jamii inayomzunguka.
Akizungumza katika semina ya mazoezi na waandishi wa habari Waziri Wa Afya maendeleo ya Jamii
Jinsia,wazee na watoto jijini dare es salaam mapema wiki hii Ummy Mwalimu,alisema watu wengi
huchukulia mazoezi ni jambo la kusema kuwa kuna wale wanaofanya kazi kwa muda mrefu na
wamebanwa wanatakiwa kutenga angalau dakika ishirini kwa siku kwa kufanya mazoezi ili kuweka mwili katika viwango bora vya ukuaji na kufanya mwili kukuwa kwa utaratibu bila kuathiri afya ya mtu.
Na inaelezwa asilimia kubwa ya magonjwa yasiyokuwa yakuambukiza husababishwa na ulaji mbovu na kutoufanyisha mwili mazoezi mara kwa mara na asilimia 60%ya vifo vyote hapa nchini husababishwa na magonjwa yasiyokuwa yakuambukiza na asilimia 40% ndio husababishwa na magonjwa ya kawaida magonjwa hayo yasiyokuwa yakuambukiza ni saratani ya utumbo mpana,homa ya ini,kisukari,kujaa mafuta katika mishipa ya damu na kufanya mzunguko wa damu mwilini kuwa mgumu hali inyopelekea mshipa huo kupasuka na kupasuka gafla na magonjwa mengine mengi.
Wafanyakazi wa CRDB Bank wakifanya mazoezi katika ufukwe wa Jimkhana |
Aliendelea kwa kusema kuwa magonjwa hayo yatepukika kwa kufanya mazoezi tu kitu ambacho kila mtu anakiweza bila kutumia garama yeyote katika kufanikisha hili.watu wengi hudhani mazoezi ni lazima ubebe chuma ,matofali au zege kitu ambacho sio sahihi bali hata kutembea ni mazoezi muhimu kuliko mazoezi yeyote.alisema Ummy.
Lakini sambamba na mazoezi hayo inatakiwa kula chakula bora hasa mboga za majani na matunda ,kuepuka ulevi wa pombe na inashauriwa mwanamke kunywa chupa moja ya pombe aina ya bia na mwanaume anatakiwa kutumia chupa mbili tu na haitakiwi kuzidisha zaidi ya hapo na kuepuka uvutaji wa tumbaku hivi ni vitu vitasaidia kuweka mwili vizuri na kuepusha mwili dhidi ya magonjwa kawaida kitu ambacho sio sahihi na kuongeza kuwa mwili unahitaji kufanyiwa mazoezi ili kuimarika zaidi.
``mtu unatakiwa kufanya mazoezi ya kutembea au kukimbia angalau kwa wiki mara tatu,na kushauri
kuwa kwa wale wanaofanya kazi katika ofisi mbalimbali wawe na desturi ya kuacha magari yao katika maegesho ya mbali na kwenda ofisini kwa miguu”alisema Ummy.
Naye mtaalamu wa mazoezi Waziri Ndonde aliyekuwa katika semina hiyo alisema suala la mazoezi sio kitu cha kuchukulia mzaa kwani ni bora ukajikinga na magonjwa mbalimbali na kufanya afya yako kuwa bora na kuishi maisha ya furaha zaidi. Pia kufanya mazoezi humweka mtu kuweza kumudu shughuli zake za kila siku bila bugudha yeyote kitu ambacho unakuwa umeliletea Taifa f maendeleo na kwa mtu binafsi pia lakini kufanya mazoezi
huufanya mwili kuwa mwepesi kwani wakati wa kufanya mazoezi mwili hutoa sumu mbalimbali kwa njia ya jasho.
Lakini pia humwongezea mtu uwezo wa kufikiri kwa wepesi na kufanya maamuzi sahihi kwa wakati
sahihi pia aliendelea kushauri pia utumiaji wa mboga za majani ni muhimu ili kufanikisha mazoezi yako yawe mazuri zaidi.
Ikumbukwe kwamba suala la ufanyaji wa mazoezi ni jukumu la kila mtu ili tuweze kuishi maisha marefu ya amani na furaha zaidi tushirikiane na Waziri wa Afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto katika kampeni yake ya mazoezi kwa nchi nzima kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae pia.kwani kinga ni bora kuliko tiba.
Post a Comment